Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM yataka mageuzi katika kikosi cha polisi Kenya

Ripoti ya UM yataka mageuzi katika kikosi cha polisi Kenya

Karibuni wapendwa wasikilizaji katika makala yetu ya ripoti ya wiki leo tutazungumzia ripoti ya mjumbe maalum wa UM kwa ajili ya mauwaji ya kiholela, inayo toa mwito kwa Rais wa Kenya kutambua na kuchukua hatua za kukomesha kile alichokieleza ni "mauwaji yanayopangwa, yaliyoenea na kufanywa kwa ustadi" na polisi wa nchi hiyo.

Mjumbe maalum wa UM Philip Alston alifanya uchunguzi wa siku kumi nchini Kenya na kusema kunahitajika uwongozi thabiti juu ya suala hili na unahitaji kutoka kinara na mageuzi makubwa katika kikosi cha polisi yanabidi kuanza kwa kumfukuza mkuu wa polisi. Nimezungumza na naibu mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya Hassan Omar na kumuliza kwanza jinsi watu walivyoipokea ripoti hiyo nchini humo