Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji 6 wazama nje ya Pwani ya Yemen

Wahamiaji 6 wazama nje ya Pwani ya Yemen

Inaripotiwa kwamba watu 6 wamefariki na wengine 11 hawajapatikana na huwenda wamefariki baada ya wafanyabishara wa magendo kuwalazimisha abiria kuchupa baharini njee ya pwani ya Yemen wiki iliyopita.

Hilo ni tukiyo la tatu hadi hivi sasa kwa mwaka huu kufuatana na Shirika la wakimbizi la UM. Msemaji wa UNHCR Ron Redmon alisema walonusurika wamesema boti lao liliondoka Alhamisi kutoka Suweto katika jimbo la Bossasso Somalia, likiwa limepakiza wa-Somalia na Wa-Ethopia 52 kuwavukisha Ghuba ya Aden, na lilikua moja kati ya maboti saba ya biashara haramu kusafirisha watu yaliyofika pwani ya Yemen siku ya Ijuma.