Skip to main content

ICTR yafungua Vituo vya Habari Rwanda

ICTR yafungua Vituo vya Habari Rwanda

Mahakama ya UM ya uhalifu wa vita vya Rwanda huko Arusha ICTR, imefungua vituo viwili vya habari kusini mwa nchi hiyo.

 Vituo hivyo ni sawa na vingine 10 vilivyofunguliwa sehemu mbali mbali ya nchi hiyo ili kuweza kutoa habari kuhusiana na mauwaji ya kimbari ili kuhamasisha amani na usalama katika eneo hilo. Alipofungua kituo cha kwanza mwezi Novemba, Registar wa ICTR Adarna Dieng alisema ni matumaini yao kwamba ujuzi na maarifa ya mawakili katika mahakma ya mikoa yataongezeka kutokana na kupata na kutumia vyanzo na teknolojia watakapoata kkatika vituo hivyo.