Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za kulinda amani, kukaguliwa kwa kina wakati inakabiliwa na upungufu wa rasilmali

Shughuli za kulinda amani, kukaguliwa kwa kina wakati inakabiliwa na upungufu wa rasilmali

Kazi za kulinda amani za UM zinazokabiliwa na hali ambayo hayajapata kutokea na upungufu mkubwa wa rasilmali, zitakaguliwa kwa kina mnamo maka unaokuja kufuatana na mkuu wa Idara ya Kazi za Kulinda Amani DPKO.

Akizungumza kwa mara ya kwanza mbele ya kamati maalum ya kulinda amani ya Baraza Kuu la UM tangu kuchukua nafasi ya Jean-Marie Guehenno, naibu KM Alain Le Roy alisema 2009 utakua mwaka muhimu sana kwa kazi za kulinda amani. Alisema kazi hazijapungukiwa kwa upande wa ukubwa na idadi ya afisi zake tu ambazo kwa ujumla ni afisi 18 kukiwepo walinda amani elfu 112, bali pia kwa upande wa changamoto zilizopo kutokana na kazi ngumu na matatizo ya vifaa na uchukuzi pamoja na mazingira ya usalama. Alisema miongoni mwa changamoto ni haja ya kutumia nguvu kuwalinda raia katika ameneoi yaliyozingwa na vita kama vile Darfur na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Bw Le Roy alisema kufanyika uchambuzi zaidi ni lazima katika kuangalia mbele lakini inabidi pia kuendelea kutekeleza majukumu na kuimarisha kwa kiwango kikubwa uwezo wao.