Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM ahimiza mataifa kutanzua tofauti zao katika vita dhidi ya ubaguzi

Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM ahimiza mataifa kutanzua tofauti zao katika vita dhidi ya ubaguzi

Kamishina mkuu wa Haki za Binadamu wa UM Navi Pillay alisisitiza jana haja ya nchi wanachama kuweka kando tofauti zao na kufanya kazi pamoja kuushinda ubaguzi wa rangi, na chuki dhidi nya wageni kabla ya mkutano wa pili wa Durban baadae mwaka huu.

Mkutano huo utakaofanyika mwezi April huko Geneva utatathmini maendeleo yaliyopatikana kote duniani tangu mwaka 2001 wakati wa mkutano wa viongozi dhidi ya ubaguzi huko Durban Afrika Kusini. Katika taarifa aliyowapelekea wajumbe wanaotayarisha mkutano huo wa Geneva, Bi Pillay alitoa mwito kwa serekali zote kutoruhusu suala lolote lile kugubika majadiliano ya umuhimu mkubwa kwa heshima ya binadamu kwa kuwatenge na kuangamizwa wengine. Sehemu ya pendekezo la mswada wa hati itakayotumiwa kama msingi wa majadiliano kwenye mkutano imekua na utata mkubwa kwa sababu ya kukosoa sera za Isael katika ardhi inazokalia za Wapalestina. Kamishina mkuu, alipendekeza pia kuandaliwa kwa warsha kadhaa kuzisaidia serekali kuweza kuafikiana ju ya suala la kukashifu dini mbali mbali.