Skip to main content

Wanachama wa OIF wakutana kutathminia maendeleo ya kuimarisha ujuzi wa kusoma na kuandika

Wanachama wa OIF wakutana kutathminia maendeleo ya kuimarisha ujuzi wa kusoma na kuandika

Kadhalika, kuanzia tarehe 11 mpaka 13 Februari (2009) watakutana kwenye mji wa Lyon, Ufaransa wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayohusika na maendeleo ya ilimu, pamoja na wajumbe wa mashirika yasio ya kiserikali kutoka zile nchi 54 wanachama wa Shirika la Mataifa Yenye Kutumia Lugha ya Kifaransa (OIF).

kutano ulitayarishwa na Serikali ya Ufaransa, ikishirikiana na Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), na mada ya majadiliano itasisitiza zaidi juu ya itikadi ya kitaaluma yenye kusisitiza kwamba maarifa hayapatikani kwa mkumbo mmoja tu, bali hujiri kwa kiawamu, katika kipindi kizima cha maisha ya mwanadamu. Mkutano utafanyisha tathmini ya taratibu za kudumisha na kusarifisha ujuzi wa kusoma na kuandika, pamoja na kupiga vita hali ya kujua kusoma na kuandika kwa kiasi kidogo. Mkutano huu unafanyika kabla ya kikao cha sita, cha kimataifa juu ya ilimu ya watu wazima, kitakachowakusanyisha wajumbe wa kimataifa mwezi Mei, mwaka huu nchini Brazil.