Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yaongoza Mkutano wa Mwaka kuhusu Matumizi ya Teknolojiya ya Kisasa ya Mawasiliano

UNICEF yaongoza Mkutano wa Mwaka kuhusu Matumizi ya Teknolojiya ya Kisasa ya Mawasiliano

Mkutano wa mwaka wa UM kuhusu matumizi ya teknolojiya ya mawasiliano ya kisasa, kwa maendeleo, umefunguliwa rasmi hapa Makao Makuu Ijumatano ya leo. Kikao hiki cha tano, kinasimamiwa na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) na majadiliano ya mkutano yanatazamiwa kuendelea hadi Ijumaa, Februari 13 (2009).

Mkutano unahudhuriwa na viongozi wanaoratibu mawazo ya kisasa pamoja na wabuni wa ufundi wa mawasiliano ya karne ya 21 wanaowakilisha UM, vyuo vikuu, sekta za binafsi na zile sekta zinazohusika na miradi ya kukuza maendeleo. Majadiliano yanatarajiwa kulenga zaidi juu ya umuhimu wa kushirikiana katika matumizi ya teknolojiya mpya ya mawasiliano, itakayosaidia kuyatekeleza, kipamoja, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia, kwa wakati.