Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali zinazozuilika zaua mamia elfu ya watoto kila mwaka, UM imeonya

Ajali zinazozuilika zaua mamia elfu ya watoto kila mwaka, UM imeonya

Ripoti iliotolewa bia wiki hii na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Mfuko wa Kimataifa juu ya Maendeleo ya Watoto (UNICEF) imebainisha ya kwamba zaidi ya watoto 2,000 wanauliwa kila siku, na majeraha wanaopata kutokana na ajali zinazozuilika, na makumi milioni ya watoto wengine, husumbuliwa kila mwaka na majeraha ambayo mara nyingi huwalemaza kimaisha.