Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa haki za binadamu kimataifa wahitajia bidii ziada, asema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu

Utekelezaji wa haki za binadamu kimataifa wahitajia bidii ziada, asema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu

Jumuiya ya kimataifa pia mwaka huu inaadhimisha waraka muhimu wa kihistoria, unaojulikana kwa umaarufu kama Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, waraka ambao tarehe ya leo umetimiza miaka 60 tangu kupitishwa na Baraza Kuu.

“Siamini kuna nchi yeyote ulimwenguni sasa hivi, inayoweza kujigamba na kudai kuwa imeshakamilisha utekelezaji wa haki za binadamu kwa umma wote kijumla, wakati makumi milioni ya walimwengu, katika sehemu mbalimbali za dunia, hata hawajatambua bado ya kwamba wamejaaliwa haki hizo, na kwamba vipo vyombo vya kisheria ya kimataifa vilivyowajaalia uwezo wa kudai kutekelezewa haki za kimsingi, bila shuruti, na kwamba Serikali zao pia zinawajibika kuzitunza haki hizo kwa kila raia, pamoja na kuimarisha haki kadha nyengine za kitaifa na kimataifa.”

Kwa mujibu wa Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, liliopitishwa na Baraza Kuu la UM mnamo tarehe 10 Disemba 1948, kwa ufupi linasema kila raia ana haki ya kuishi, kwa uhuru na kwa amani – na watu wote, wana haki sawa chini ya sheria, bila kujali kabila, jinsiya, rangi, lugha, dini na itikadi, au maoni ya kisiasa.