Hapa na Pale

2 Oktoba 2008

Zhang Yesui Mjumbe wa Kudumu wa Uchina katika UM atachukua uongozi wa Uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba, baada ya Michel Kafando, Mjumbe wa Kudumu wa Burkina Faso kumaliza muda wa Mwenyekiti wa Baraza kwa mwezi Septemba.

Vikosi vya UM vinavyolinda amani katika JKK (MONUC) vimetumia helikopta ziliopiga makombora, katika eneo la mashariki, baada ya waasi wa FRPI katika jimbo la Ituri walipodunga risasi ndege ya upelelezi ya UM, walipokuwa wanajaribu kusonga mbele kwenye mapigano dhidi ya vikosi vya Serikali. Mashambulio haya ya UM ni ya pili dhidi ya waasi kufuatilia lile shambulio liliotukia wiki mbili nyuma kusini, katika jimbo la Kivu Kaskazini. Mabaki ya waasi wa FRPI, walianza mashambulio yao Ijumatatu dhidi ya vikosi vya Serikali na kuteka kambi mbili; na baadaye walijaribu kuelekea kwenye kijiji cha Aveba. Lakini shambulio la helikopta za MONUC ziliwazuia kusonga mbele.

KM Ban Ki-moon alipohutubia mkutano kuzingatia mahitaji ya nchi zinazoendelea zisio na bandari alisema ni muhimu kwayo kuongeza wingi wa bidhaa zinazosafirishwa nje, ili kuziwezesha kutekeleza, kwa wakati, Malengo ya Maendeleo ya Milenia. KM aliitaka jamii ya kimataifa kuonyesha ukarimu mkuu kuzisaidia nchi 31 zisio na bandari, ili kudhibiti tatizo la kutengwa kibiashara, kwa mchango maridhawa sawa na ule ulioahidiwa Mataifa maskini wiki iliopita uliokusudiwa kuyakamilisha malengo ya maendeleo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter