Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu awatetea waliowekwa kwenye vifungo onevu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu awatetea waliowekwa kwenye vifungo onevu

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, Alkhamisi alifanyisha mahojiano ya awali Geneva na waandishi habari tangu kuanza kazi. Miongoni mwa masuala muhimu aliyoyaangaza na kutilia mkazo zaidi kwenye kikao hicho, ilikuwa ni lile suala linalohusu mradi mpya utakaoanzishwa na ofisi yake unaojulikana kama Mradi wa Kuimarisha Hishima na Haki kwa Watu Waliowekwa Kizuizini.

'Kuhusu usuli wa huu mradi ulioanzishwa na Ofisi yangu, ningelipendelea kusema hii ni hatua iliochukuliwa kwa kuambatana na taadhima za miaka 60 tangu Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu lilipoidhinishwa. Tungelipendelea kuona mradi wetu unazingatiwa, kwa uangavu mkubwa, na taasisi za kitaifa zinazohusika na haki za binadamu, zikijumlisha pia yale mashirika yasio ya kiserikali (NGOs) pamoja na wadau wengine, na hasa vyombo vya habari, ambao wote wanatakiwa wasailie, kwa makini zaidi na kusaiada kueneza taarifa kuhusu haki za watu walionyimwa uhuru wao, wanaojikuta wamevumbikwa na kuselelea kwenye magereza, na katika vizuizi vyengine vya kitaifa na kimataifa, wakikoseshwa haki halali ya kufikishwa mahakamani kujitetea dhidi ya kifungo onevu. Mradi wa Kuhishimu Haki ya Watu Waliowekwa Kizuizini Bila Hukumu umekusudiwa kuhakikisha sheria ya kimataifa inatekelezewa umma huu kwa kila njia.'