Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM na Kiongozi wa Ufaranza wahimiza hatua ya dharura kutatua mzozo wa fedha

KM na Kiongozi wa Ufaranza wahimiza hatua ya dharura kutatua mzozo wa fedha

Ijumamosi iliopita KM Ba Ki-moon alikutana na Raisi wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 12 wa Mataifa Yanayotumia Lugha ya Kifaransa Mjini Québec, Kanada, ambapo wote wawili walitilia mkazo rai ya kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa, kukabili kipamoja mzozo wa fedha uliojiri ulimwenguni kwa sasa hivi.