Kamati ya Mipaka Sudan inafadhiliwa na UM vifaa vya kupimia kwa satalaiti
Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan anayeongoza Shirika la la UM la UNMIS, Ashraf Jehangir Qazi ameikabidhi Kamati ya Maalumu ya Ufundi wa Kuweka Mipaka vifaa vya kutengeneza ramani vinavyotumia satalaiti, ikiwa moja ya pendekezo muhimu liliojumlishwa kwenye Mapatano ya Jumla ya Amani yaliosaidia kusitisha mapigano ya muda mrefu baina ya maeneo ya kaskazini na kusini Sudan.