UM una wasiwasi juu ya marekibisho ya haki ya kupata hifadhi kwa wahamiaji Yemen

21 Oktoba 2008

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamaiji (UNHCR) limeiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemen iipatie UM fafanuzi halisi kuhusu tangazo lenye kudai wahamiaji wa kutoka Ethiopia na Eritrea hawatoruhusiwa tena kuingia nchini.

"Ofisi ya UNHCR katika Yemen imeiomba serikali iipatie ufafanuzi kuhusu taarifa za karibuni za Wizara ya Mambo ya Ndani ya kwamba hawatoruhusu tena raia wa Eritrea na Ethiopia kuingia nchini." Alisema taarifa hiyo ilitolewa wakati mmoja na baada ya kuanzishwa tena magendo ya kuvusha watu kwenye Ghuba ya Aden kutokea eneo la Pembe ya Afrika, fungu kubwa lao likiwa wahamiaji wa kutokea Usomali, na vile vile baadhi yao kutoka Ethiopia, Eritrea na mataifa mengineyo. Alikumbusha Msemaji wa UNHCR ya kwamba Yemen ni taifa lilioidhinisha Mkataba wa Kutoa Hifadhi kwa Wahamiaji wa 1951, chombo cha sheria ya kimataifa ambacho kinaliwajibisha taifa pokezi kutoa hifadhi kwa wahamiaji kwa mwonekano wa kwanza, kama Yemen inavyowafanyia raia wa Usomali, na pia raia wa mataifa mengine ambao walipokuwa wakiomba hifadhi walipatiwa kibali katika siku za nyuma bila matatizo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter