Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya biashara na Umoja wa Mataifa wanazingatia kipamoja utunzaji wa hali ya hewa

Mashirika ya biashara na Umoja wa Mataifa wanazingatia kipamoja utunzaji wa hali ya hewa

Wawakilishi kutoka mashirika makuu ya biashara 150, ikijumlisha pia wajumbe wa jumuiya za kiraia na serikali kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika Ijumanne ya leo Geneva kwenye mkutano unaoungwa mkono na UM, kusailia suluhu za kutoka wafanyabiashara zitakazotumiwa kupambana na matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayopaliliwa na uharibifu wa mazingira.