Skip to main content

UM inaadhimisha Siku ya Kimataifa juu ya Ujuzi wa Kusoma na Kuandika

UM inaadhimisha Siku ya Kimataifa juu ya Ujuzi wa Kusoma na Kuandika

Tarehe 08 Septemba inaadhimishwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Ujuzi wa Kusoma na Kuandika. Mada ya taadhima ya mwaka huu imetilia mkazo fungamano ziliopo kati ya uwezo wa mtu kusoma na kuandika na afya bora.

Utafiti umethibitisha, kwa kurudia mara kadha, kuwepo uwiano mkubwa kati ya afya bora na ujuzi wa kusoma na kuandika kwa mwanadamu. Mathalan, uchunguzi ulioendelezwa katika nchi 32 umethibitisha kihakika wanawake waliopata elimu ya sekondari huwa wamearifika, mara tano zaidi, kuhusu hatari ya maambukizo ya VVU/UKIMWI kuliko wale wasiojua kusoma wala kuandika. Mfano mwengine: viwango vya vifo vya watoto wachanga miongoni mwa mama wasiojua kusoma wala kuandika ni vikubwa zaidi.

Koïchiro Matsuura, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwenye taarifa alioiwasilisha kuihishimu Siku ya Kimataifa ya Ujuzi wa Kusoma na Kuandika alisema “mtu asiyejua kusoma wala kuandika anakabiliwa na hatari kuu ya kupatwa na maradhi, na ana fursa chache ya kutafuta huduma za afya kwake yeye binafsi, aila yake na hata jamii zao.”