Kamishna Mkuu mpya wa Haki za Binadamu asisitiza, ubaguzi ukikomeshwa mauaji ya halaiki yatasita duniani
Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Jaji Navanethem Pillay, Ijumatatu alihutubia, kwa mara ya kwanza tangu kuchukua madaraka 01 Septemba (2008), Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswiss.