Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Operesheni za chakula Darfur zadhuriwa na mashambulio ya kihorera

Operesheni za chakula Darfur zadhuriwa na mashambulio ya kihorera

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetoa taarifa inayotahadharisha jumuiya ya kimataifa ya kuwa italazimika kukatisha operesheni za kugawa chakula, kwa muda, katika baadhi ya sehemu za Darfur, Sudan mpaka pale hali ya usalama na utulivu itakaporejea.