Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO itawasaidia wakulima Swaziland kujikimu bora kimaisha

FAO itawasaidia wakulima Swaziland kujikimu bora kimaisha

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza Ijumatatu kuanzisha mradi wa kuwafadhilia wakulima masikini wanaojikimu chakula katika ufalme wa Swaziland, kusini mwa Afrika, vocha maalumu zitakazowawezesha wao kununua mbegu kutoka soko la kitaifa na kuhakikisha wanapanda mbegu hizo katika majira yanayofaa.