Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Vikosi vya Ulinzi Amani vya UM katika JKK (MONUC), vikisaidiwa na helikopta za vita Ijumaa walishambulia wafuasi wa kundi la waasi wa CNDP kwenye mji uliopo eneo la mashariki, kilomita 60 kutoka mji wa Goma. Waasi hao walikuwa wanaelekea jimbo la Kivu Kaskazini kwa madhumuni ya kuuteka mji baada ya kutangaza kabla dhamira yao hiyo. Shambulio la vikosi vya MONUC liliwalazimisha kurudi nyuma na kukatiza lengo lao.~~

UNICEF imeripoti kwamba imefanikiwa kuwapatia watoto 142,000, baina ya umri wa miezi 9 hadi miaka 15 katika Usomali chanjo dhidi ya surua katika mji wa Mogadishu na kwenye zile kambi za watu waliong’olewa makazi katika Afgoye, licha ya kuwa hali ya usalama kijumla nchini bado ni ya kutia wasiwasi, na fujo inaendelea kusumbua raia. Kwa mujibu wa takwimu za UM maradhi ya shurua ndio ugonjwa unaosababisha idadi kubwa ya vya watoto katika Usomali.

Ijumaa, Baraza la Haki za Binadamu lilitumia siku nzima kuzingatia suala la ubaguzi wa rangi, ukabila na kwa kina ile tabia ya kukashifu dini tofauti. Githu Muigai, Mkariri/Mtaalamu Maalumu anayeshughulikia haki zinazotenguliwa na ubaguzi wa rangi wa kisasa, pamoja na chuki za wageni na utovu wa ustahamilivu aliwakilisha ripoti yake ya awali mbele ya Baraza, iliosailia tabia karaha za kukashifu dini, hususan athari haribifu zinazoambatana na khofu za chuki dhidi ya UIslam.