WHO inasema sigara ya elektroni si tiba ya kukomesha uvutaji sigara
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tangazo maalumu lenye kutahadharisha juu ya hatari ya kutumia ile sigara ya elektroni, ambayo watangazaji wa biashara wanadai humpatia mvutaji tiba ya kuwacha kuvuta sigara za kawaida. Kwa mujibu wa WHO madai haya hayana msingi na hayajathibitishwa kisayansi,na kuwataka wachuuzi wa sigara za elektroni waache kudai WHO imeidhinisha matumizi ya sigara hizo.