'Vifo vya uzazi katika nchi maskini ni msiba usiostahamilika' imehadharisha UNICEF
Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) umetoa ripoti juu ya vifo vya uzazi ambavyo hukutikana zaidi miongoni mwa mama waja wazito katika mataifa yanayoendelea. Ripoti iliopewa mada isemayo “Maendeleo ya Watoto: Fafanuzi juu ya Udhibiti wa Vifo vya Uzazi” ilibainisha kwamba asilimia 99 ya vifo vya uzazi hutukia zaidi katika nchi zinazoendelea, na kati ya idadi hiyo asilimia 84 humakinikia kwenye zile nchi ziliopo kusini ya Sahara na Asia ya Kusini. Mkuu wa Afya wa UNICEF, Dktr Peter Salama aliwaambia waandishi habari Geneva umuhimu wa ripoti.