Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaadhimisha Siku ya Amani Kimataifa

UM unaadhimisha Siku ya Amani Kimataifa

Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Amani Kimataifa kwa kuandaa tafrija kadha wa kadha zilienedelezwa katika Makao Makuu mjini New York, na kwenye maeneo mengine ya dunia. KM Ban Ki-moon alijumuika na watu mashuhuri kadha walioteuliwa kama Wajumbe wa Amani wa UM, pamoja na Raisi wa Baraza Kuu na watumishi wa UM kwenye tafrija maalumu ya kila mwaka ambapo KM aligonga kengere ya amani iliopo kwenye bustani ya UM.

Siku ya Amani Kimataifa huadhimishwa kila mwaka katika tarehe 21 Septemba. Lakini ilivyokuwa mwaka huu siku hiyo inaangukia Ijumapili UM umeamua kuiadhimisha Ijumaa ya leo, Septemba 19 (2008).