Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Raisi Omar al-Bashir wa Sudan alipozuru mji wa El Fasher katika Darfur, alipata fursa ya kukutana, kwa muda mfupi na Mjumbe Maalumu wa Pamoja kwa Darfur wa UM/UA, Rodolphe Adada pamoja na viongozi wengine wa shirika la mchanganyiko la UM-UA linalosimamia ulinzi wa amani katika Darfur (UNAMID).

Kwa mujibu wa taarifa za UM Raisi wa Sudan aliahidi viongozi wa UNAMID kwamba serikali yake ipo tayari kuwapatia kila hifadhi watumishi wa shirika wao pamoja na misafara yao ya ulinzi. Kadhalika UNAMID imeripoti kusita zile shughuli za kuwapeleka kwenye uhamisho wa muda wale wafanyakazi wasio wa lazima kutoka Darfur. Huduma hizo zilisita Ijumaa tarehe 18 Julai baada ya jumla ya watu 300 kuhamishiwa kwenye mataifa jirani wakisubiri hali ya mamo kieneo.

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limearifu makundi fulani yenye silaha, katika jimbo la Ituri, yalikutikana kuvunja sheria ya kusitisha mapigano mwanzo wa wiki. Imeripotiwa makundi mawili yenye silaha yalishiriki kwenye mapigano ya bunduki katika mji wa Tchey, na hayakusitisha uhasama mpaka baada ya vikosi vya UM kuingilia kati. Ripoti zilisema hakuna aliyejeruhiwa na tukio hilo. Kadhalika, kwenye eneo la Kivu Kusini MONUC imeripoti walinzi amani wa UM walilazimika mara tatu kuingilia kati na kusitisha mapigano ya bunduki kati ya makundi ya kizalendo yanayohasimiana.