Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

BU inazingatia hali mbaya ya wahamiaji Chad na CAR

BU inazingatia hali mbaya ya wahamiaji Chad na CAR

Ijumatano Baraza la Usalama (BU) lilikutana kwenye kikao cha faragha kuzingatia hali katika Chad na kaskazini-mashriki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Aprili, Balozi Dumisani Kumalo wa Afrika Kusini baada ya mkutano alizungumza na waandishi habari wa kimataifa na aliwalezea ya kwamba wajumbe wa Baraza wanashtumu, kwa kauli moja, vitendo vya kutumia silaha na mabvu vilivyotukia Chad mashariki na kuthibitishwa kuwa vilishadidiwa na makundi ya waasi.