Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame mkali wadhuru sana mavuno ya mahindi Zimbabwe, FAO inaonya

Ukame mkali wadhuru sana mavuno ya mahindi Zimbabwe, FAO inaonya

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limetoa ripoti inayohadharisha kwamba ukame mkali uliovamia karibuni majimbo kadha ya Zimbabwe, unaashiriwa kukuza madhara makubwa kwa mavuno ya mahindi mwaka huu. Ripoti ilibainisha wasiwasi wa FAO ya kuwa hali hii huenda ikapalilia zaidi mazingira magumu yaliotanda sasa hivi katika taifa hili la kusini ya Afrika.