Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa FAO ahimiza hatua za dharura kudhibiti mfumko wa bei za chakula ulimwenguni

Mkuu wa FAO ahimiza hatua za dharura kudhibiti mfumko wa bei za chakula ulimwenguni

Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) Ijumatano aliwaambia wajumbe wanaohudhuria kikao cha awali cha Mkutano wa Viwanda vya Mavuno ya Kilimo Ulimwenguni mjini New Delhi, Bara Hindi kwamba walimwengu wanatakiwa kuchukuwa hatua za dharura, kipamoja, ili kuhakikisha zile athari mbaya, za muda mfupi, zinazochochewa na muongezeko wa bei za chakula duniani, hazitoendelea kukandamiza na kuumiza fungu kubwa la watu muhitaji masikini na mafakiri wanaoishi katika nchi zinazoendelea.