Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laridhika na maendeleo ya utaratibu wa amani Uganda.

Baraza la Usalama laridhika na maendeleo ya utaratibu wa amani Uganda.

Baraza la Usalama la karibisha maendelo mazuri yaliyopatikana hivi karibuni katika utaratibu wa amani kati ya serekali ya Uganda na waasi wa Lord Resistance Army LRA, na kutoa mwito kwa pande zote mbili kutumia kila nafasi zilizo jitokeza kuendelea mbele na kuboresha maisha ya wakazi wa kaskazini ya Uganda.

Wajumbe wa baraza walirudia tena uungaji mkono wao wa kupatikana suluhisho kupitia majadiliano na kueleza matumaini ya kufikiwa makubaliano ya haraka. Mjumbe maalum wa katibu mkuu kwa ajili ya amani ya Uganda Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano aliliarifu baraza la usalama wiki hii juu ya maendeleo hayo. Na kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 20 waasi wa LRA walifika Kampala na kua na mazungumzo na Rais Yoweri Museveni na maafisa wengine wa serekali. Na kwa wakati huu wajumbe wa waasi wanatembelea sehemu mbali mbali za nchi na kushauriana na wananchi juu ya hatua za kuendelea mbele.