Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya amani vya UM na Umoja wa Ulaya kupelekwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Vikosi vya amani vya UM na Umoja wa Ulaya kupelekwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baraza la Usalama limepitisha azimio muhimu lilioruhusu vikosi vya ulinzi wa amani vya UM na Umoja wa Ulaya kupelekwa katika Chad mashariki na sehemu za mashariki-kaskazini ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Vikosi hivi vinatazamiwa kuwapatia raia wa maeneo hayo hifadhi, na vile vile kuwapatia wahamiaji na umma uliong’olewa makwao ulinzi bora dhidi ya mashambulio ya kihorera.

Vikosi vya UM/Umojawa Ulaya vitakuwa na majukumu mbalimbali, na vinatazamiwa kuendesha operesheni zao kwa kuambatana na Kifungu cha Saba cha Mkataba wa UM, ambapo wataruhusiwa kutumia silaha kulinda usalama wa watumishi na vifaa vya UM. ‘Shirika’ hili jipya la ulinzi wa amani katika Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati litajulikana kama Shirika la MINURCAT.