Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamisheni ya CSD imeanzisha mjadala wa mwaka Makao Makuu

Kamisheni ya CSD imeanzisha mjadala wa mwaka Makao Makuu

Kamisheni ya Baraza Kuu juu ya Maendeleo ya Kudumu (CSD), mnamo tarehe 30 Aprili (2007)imeanzisj kika cha mwaka kwenye Makao Makuu ya UM, ambapo wajumbe 2000 ziada, wakiwakilisha mataifa wanachama pamoja na wataalamu kadha kutoka kanda mbalimbali za kimataifa, walijiandaa kuzingatia suluhu ya muda mrefu kuhusu tatizo la nishati, kwa matarajio ya kukuza maendeleo ya, hasa, mataifa masikini, ikiwa miongoni mwa juhudi za kuyapunguzia mataifa yanayoendelea athari za kiuchumi na jamii kutokana na umwagaji wa hewa chafu angani.

Kadhalika, Tume ya Serekeli za Kimataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (IPCC), iliokutana kwenye wa Bangkok, Thailand wiki hii imethibitisha kwamba jamii ya kimataifa ina uwezo wa kupunguza kasi, na halafu kudhibiti tatizo la umwagaji wa hewa chafu dhidi ya mazingira katika miongo ijao, yaani zile gesi zinazojulikana kwa umaarufu kama gesi za CHGs. Uchafuzi huo unaweza kurudishwa nyuma na kudhibitiwa vlivyo pindi walimwengu wataanza kutumia teknolojia za kisasa na kutekeleza sera za dharura ambazo natija zake zinalingana na gharama.

Miongoni mwa nasaha zilizopendekezwa na Tume ya IPCC zitakazosaidia kupunguza uharibifu wa hewa na mazingira ni ile rai ya kutumia gesi asilia na nishati yenye uwezo wa kutumiwa mara kwa mara na kuikwepa petroli au ile nishati inayoambatana na aina ya kaboni. Kadhalika nchi wanachama zilinasihiwa kuacha kuangamiza misitu na kujaribu kutumia teknolojia safi katika viwanda ili kuepukana na tatizo la kumwaga hewa chafu angani.