Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Waundaji sera za kitaifa pamoja na wataalmu kutoka ulimwengu wa taaluma, sayansi na biashara wamekutana mjini Trieste, Utaliana kwenye mkutano wa siku tatu, ulioandaliwa na mataifa ya G-8 pamoja na UNESCO, kuzingatia hatua za kuchukuliwa kimataifa kuhamasisha maendeleo ya kudumu, kwa kutumia mfumo wa kufungamanisha matumizi ya uvumbuzi wa teknolojia ya kisasa, utafiti wa kisayansi na ilimu.

Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) Alkhamisi limewasilisha ripoti kamili yenye kuthibitisha, kihakika, tatizo la kuselelea kwa fujo, takriban duniani kote, kwa vitendo vya ubaguzi wa kijinsia dhidi ya wanawake katika mahali pa kazi.

UNICEF imepongeza tangazo la Wakf wa Raisi Mstaafu wa Marekani Bill Clinton la kufikia makubaliano na makampuni ya madawa ya Cipla na Matrix, na kupunguza bei ya zile dawa 16 muhimu za tiba ya VVU/UKIMWI; maafikiano haya yatawasaidia kurefusha maisha mamilioni ya watoto wagonjwa wa UKIMWI katika mataifa yanayoendelea.