Mradi wa kudhibiti homa ya manjano kuanzishwa na WHO Afrika Magharibi

18 Mei 2007

Baraza Kuu la Shirika la Afya Duniani (WHO), ambalo linakutana sasa hivi Geneva, Uswiss limepitisha mradi wa kuanzisha kampeni ya kudhibiti homa ya manjano katika mataifa 12 yaliopo Afrika Magharibi. Kwa mujibu wa WHO maradhi ya homa ya manjano yaligunduliwa kuibuka katika baadhi ya sehemu za Afrika Magharibi na kunahitajika juhudi za dharura kuyadhibiti yasije yakafumka kwa kasi na kulitapakaza janga hilo kwa umma uliobanwa na matatizo kadha mengineyo ya kiuchumi na jamii.

WHO inatarajia kupokea mchango wa dola milioni 58 zitakazotumiwa kuhudumia watu milioni 48 tiba kinga dhidi ya homa ya manjano. Mradi unaungwa mkono na WHO, UNICEF na vile vile mashirika mengine ya kimataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter