Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alihimiza viongozi na wajumbe waliohudhuria kikao cha mwaka cha sita cha bodi linaloandaa sera na miradi ya afya ya kimataifa, kinachokutana hivi sasa Geneva, Uswiss kwamba kunatakikana hima kuu ya jumla kutoka kwao wote, kujenga kile alichokiita “urithi wa afya”, kadhia ambayo alitumai ikikamilishwa itasaidia kuaboresha siha za wanawake na afya ya umma wa Afrika, kwa ujumla; kwa sababu, Dktr Chan anaamini kidhati kuwa wanawake ni fungu muhimu la umma wa kimataifa, linaloongoza kwenye harakati kadha wa kadha za maendeleo ulimwenguni.

[na hatimaye] Kamati ya UM ya Kufyeka Ubaguzi wa Kijinsia dhidi ya Wanawake (CEDAW) imeanzisha kikao cha wiki mbili kufanya mapitio ya ripoti juu ya utekelezaji wa mkataba wa haki za wanawake duniani; na Kamati inatarajiwa kusikiliza ripoti zitakazowakilishwa na Mauritania, Serbia, Syria, Msumbiji, Niger, Pakistan na vile vile Sierra Leone na Vanuatu.