Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi unahitajika Bukini baada ya maafa ya tufani

Msaada zaidi unahitajika Bukini baada ya maafa ya tufani

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA)imeripoti kuwa imewajibika kuomba msaada zaidi wa dola milioni 20 kwa Bukini, kukidhia mahitaji ya kihali ya umma ulioathirika na maafa yaliosababishwa na kimbunga kilichopiga huko mnamo miezi miwili iliopita.

Kwa mujibu wa Ofisi ya OCHA akiba ya chakula Bukini imepungua sana, hususan baada ya kudhurika vibaya na ukame uliotanda kwenye sehemu kadha za nchi na kutangulia dharuba za tufani na vimbunga.