Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM kulitaka Baraza la Usalama (BU) kuanzisha mazungumzo ya amani kwa Sahara ya Magharibi

KM kulitaka Baraza la Usalama (BU) kuanzisha mazungumzo ya amani kwa Sahara ya Magharibi

Ripoti ya karibuni ya KM juu ya Sahara ya Magharibi imependekeza kwa Baraza la Usalama kuwaita Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi cha Frente Polisario, kushiriki, bila ya shuruti, kwenye mazungumzo ya kuleta suluhu ya kuridhisha, na ya kudumu, itakayoupatia umma wa Sahara ya Magharibi fursa ya kujichagulia serekali halali ya kuwawakilisha kitaifa.

Kadhalika, KM aliyahimiza makundi husika katika Sahara ya Magharibi kuondosha vikwazo vyote vinavyowazuia waangalizi wanajeshi wa UM kwenda watakapo kuendeleza kazi zao, na pia kuayataka makundi hayo yaendelee kuwasiliana na Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamau (OHCHR). KM amependekeza kwa Baraza la Usalama kuongeza muda wa Shirika la UM juu ya Usimamizi wa Kura ya Maoni Sahara Magharibi, kwa miezi sita zaidi, mapaka 31 Oktoba 2007.