Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwafaka wa kuacha mapigano Uganda Kaskazini wapongezwa na KM

Mwafaka wa kuacha mapigano Uganda Kaskazini wapongezwa na KM

KM Ban Ki-moon ameyakaribisha makubaliano ya karibuni, kati ya Serekali ya Uganda na waasi wa LRA, ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano mpaka mwisho wa Juni, na pia kuahidi kurejea kwenye mazungumzo ya amani yatakayofanyika kwenye mji wa Juba, 26 Aprili, mazungumzo ambayo yatasimamiwa na Naibu Raisi wa Serekali ya Sudan Kusini. Mazungumzo haya ya amani yalitayarishwa na Joaquim Chissano, Mshauri Maalumu wa KM juu ya mzozo wa Uganda Kaskazini.

KM ameyasifu makundi yote yanayohusika na mzozo wa Uganda kaskazini kwa kujihusisha kwenye juhudi za kurudisha amani kwenye eneo husika, na anatumai mazungumzo ya Juba yatafanikiwa kuwasilisha suluhu ya kudumu ya mzozo wao, ambao ulisababisha mateso makubwa na kuathiri maisha ya umma wa Uganda Kaskazini.