Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama Kuu ya Zimbabwe kupongezwa na UM kwa uamuzi juu ya kiongozi wa upinzani

Mahakama Kuu ya Zimbabwe kupongezwa na UM kwa uamuzi juu ya kiongozi wa upinzani

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour amenakiliwa akisema anaunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe ulioishurutisha Serekali kumruhusu kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC, Morgan Tsvangirai kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu baada ya kuthibitika kwamba alipigwa na kujeruhiwa vibaya na vikosi vya polisi alipokuwa kizuizini.

KM Ban Ki-moon alilaumu upigaji wa wafuasi wa chama cha upinzani wakati walipowekwa kizuizini. Aliinasihi Serekali ya Zimbabwe kuruhusu mkusanyiko wa raia ulio salama, na pia kuupatia umma huo fursa ya kutekeleza haki zao halali za kisiasa. Uhuru wa kukusanyika kwa utulivu wa amani, alisisitiza KM, ni haki ya kimsingi ya kideomkrasia kwa kila raia.