Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo yaripotiwa Burundi kuhusu ulinzi wa watoto walioathirika na vita

Maendeleo yaripotiwa Burundi kuhusu ulinzi wa watoto walioathirika na vita

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM kuhusu Hifadhi ya Watoto katika Mazingira ya Mapigano, alizuru Burundi wiki hii. Alisema kwamba ameshuhudia maendeleo ya kutia moyo katika juhudi za Serekali kuwapatia watoto walionaswa kwenye hali ya uhasama na vita, ulinzi bora na hifadhi inayotakikana kisheria.

Coomaraswamy alizuru Burundi kujionea mwenyewe hali ilivyo, na alilenga uchunguzi wake zaidi kwenye yale masuala yanayohusu wanajeshi mtoto, utumiaji mabavu wa kijinsiya, na kwenye tatizo la uwekaji kizuizini watoto wenye umri mdogo wanaoshirikiana na makundi ya wanamgambo.