Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wapya wa CAR wakabiliwa na changamoto nyingi- Keita-Bocoum

Viongozi wapya wa CAR wakabiliwa na changamoto nyingi- Keita-Bocoum

Mtaalam huru kuhusu haki za binadamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Marie-Thérèse Keita-Bocoum, amesema kuwa wawakilishi wapya waliochaguliwa nchini humo wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kuendeleza haki za binadamu.John Kibego na taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Bi Keita-Bocoum amesema hayo wakati wa ziara yake ya sita nchini CAR, ambapo amempongeza rais mpya, Faustin Archange Touadéra, na kumpa taarifa kuhusu hali ya haki  za binadamu, zikiwemo hatua zilizopigwa na changamoto zilizosalia.

Amemhimiza rais huyo mpya na serikali atakayoiunda kuchukua hatua madhubuti katika kutimiza matarajio ya umma katika kurejesha usalama, kupokonya silaha vikundi vilivyojihami, kuimarisha utawala wa sheria na kupambana na ukwepaji sheria, maridhiano ya kitaifa, pamoja na haja ya dharura ya kuwezesha upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii, mathalan elimu na afya.

Amesisitiza umuhimu wa viongozi waliochaguliwa kuwa watu wanaodhamiria kuwakilisha matakwa ya watu wa CAR kwa uadilifu na kwa kuheshimu haki za binadamu.