Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angelina Jolie kutembelea wakimbizi Ugiriki kwa niaba ya UNHCR

Angelina Jolie kutembelea wakimbizi Ugiriki kwa niaba ya UNHCR

Mjumbe Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Angelina Jolie-Pitt ameendelea na ziara yake akitembelea leo nchini Ugiriki kukutana na wakimbizi. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Lengo la ziara ya Angelina Jolie anayoifanya kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi ni kutathmini hali ya mapokezi na ulinzi wa wakimbizi nchini humo, hasa wanawake, walemavu na watoto wasioambatana na mzazi au mlezi wanaokumbwa na changamoto zaidi.

Aidha ataangazia jinsi gani UNHCR inaweza kuongeza msaada wake kwa serikali ya jamii za Ugiriki katika kukabiliana na mzigo huo wa wakimbizi.

Taarifa ya UNHCR imeeleza kwamba asilimia 85 ya wakimbizi wanaotafuta hifadhi Ulaya wanapitia Ugiriki, na hadi sasa, idadi yao nchini Ugiriki ni 40,000 na wanahitaji ulinzi na usaidizi wa kibinadamu.