Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lasikitishwa na kuzorota kwa usalama Burundi

Baraza la usalama lasikitishwa na kuzorota kwa usalama Burundi

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea kusikitishwa kwake kuhusu kuendelea kwa ukosefu wa usalama,  kuongezeka kwa machafuko  na misuguano nchini Burundi kunakosababishwa na kukosekana kwa majadiliano kutoka kwa wadau wa nchi hiyo.

Taarifa ya baraza hilo imesema inatambua mkutano wa baraza la usalama la muungano wa Afrika (AU) mnamo tarehe 17 Oktoba kuhusu hali nchini Burundi na tamko ikiwamo hatua pendekezwa ilyopitishwa na mkutano.

Baraza limeelezea kadhalika kusikitishwa na kuongezeka kwa visa vya uvunjifu wa haki za binadamu ikiwamo mauaji ya kujichukulia sheria mkononi , utesaji na uhalifu mwingine kiynume na ubinadamu ukiwamo ukamatwaji na uwekwaji vizuizini.

Taarifa inasema baraza linaelezea kusononeshwa na kuendelea kwa ukwepaji wa sheria dhidi ya wanahabari, na hali mbaya ya kibinadamu inayoonekana  bayana kutokana na watu 200,000 kusaka hifadhi katika nchi jirani.