Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wakutana Nairobi kujadili miji rafiki kwa watu wenye ulemavu

Wataalamu wakutana Nairobi kujadili miji rafiki kwa watu wenye ulemavu

Mkutano wa kimataifa kuhusu mjii na watu wenye ulemavu umewaleta pamoja wataalamu kuhusu upangaji miji kwa kuzingatia kundi hilo ambapo kwa zaidi ya siku tatu watajadili suluhu za kufanya maendeleo ya miji kuwa jumuishi na upatikanaji kwa kundi hilo ambalo idaidi yake ni bilioni moja kote dunaini wengi wakiishi mjini.

Mkutano huo ambao umefunguliwa leo mjni Nairobi chini ya uratibu wa idara ya masuala ya kichumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA, unalenga kusaidia nchi na wadau wengine kumuaga na kukuza miji jumuishi .

Taarifa kuhusu mkutano huo inasema kuwa matokeo tarajiwa ni mapendekezo muhimu ya ajenda ya kujenga miji jumuishi na yenye upatikanaji wa huduma kwa wote wakiwamo watu wenye ulemavu.

Mapendekezo hayo yanatarijiwa kubainisha umuhimu wa sera za miji bora na viwango vilivyoandaliwa kwa ajili ya wote. Ajenda hiyo inatarajiwa kuongoza upangaji miji duniani kwa miongo miwili.