Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wanne wa UM waliouawa Afghanistan waenziwa

Wafanyakazi wanne wa UM waliouawa Afghanistan waenziwa

Huko Afghanistan hii leo kumefanyika kumbukumbu maalum ya wafanyakazi wanne wa Umoja wa Mataifa waliouawa katika shambulio la kigaidi kwenye mji mkuu Kabul mwezi Januari mwaka huu. Kumbukumbu hiyo imeenda sambamba na uzinduzi wa bamba maalum lililonakshiwa majina ya wafanyakazi hao Vadim Nazarov wa Russia, Basra Hassan wa Marekani, Dkt. Nasreen Khan wa Pakistan na Wabel Abdallah kutoka Lebanon.

Naibu Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo na Mkuu wa ofisi ya umoja wa Mataifa UNAMA Mark Bowden aliongoza kumbukumbu hiyo akisema kuwa…

(Sauti ya Bowden)

"Kumbukumbu ya wenzetu waliopoteza maisha bado iko nasi na ni muhimu sana. Vifo vyao ni pigo kubwa siyo tu kwa Umoja wa Mataifa bali pia Afghanistan.”

Kikundi cha kigaidi cha Talibani kilikiri kuhusika na shambulio hilo lililosababisha vifo vya raia 21 na wengine wengi kujeruhiwa.