Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi waanza maisha mapya

Wakimbizi wa Burundi waanza maisha mapya

Kambi ya Mutabila iliyokuwa imewapokea wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania imefungwa rasmi tarehe 31 Mwezi Desemba mwaka jana na kuwa kambi ya mwisho kabisa kufungwa. Kambi iliyoko magharibi mwa Tanzania ilikuwa imewapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 36 Elfu wa Burundi ambao tayari wamerejea nchini mwao Burundi katika shughuli iliyosimamiwa na Shirika la kimataifa la kuwahudumia Wakimbizi UNHCR kwa ushirikiano na Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM.

Hii imefuatia azimio la pande tatu yaani serikali ya Burundi, serikali ya Tanzania na UNHCR ya kuwarejesha wakimbizi hao kwa hiari baada ya kupatikana kwa amani nchini mwao. Kundi la mwisho la raia hao wa Burundi limerejea nyumbani mwishoni mwa mwezi disemba na kutua katika kituo cha muda katika mkoa wa kusini wa Makamba.

Muandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA alifuatilia shughuli hiyo na kutuandalia makala haya.

(PKG YA RAMADHAN KIBUGA)