Mengi yanahitaji kufanywa ili kukabiliana na ulanguzi wa madawa ya kulevya:Fedotov
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana na madawa ya kulevya na uhalifu Yuri Fedotov amesema kuwa mataifa yanastahili kufanya jitihada za kukabilina na ulanguzi na mahitaji ya madawa ya kulevya.
Fedotov anesema kuwa kuzuia, matibabu na kuwasaidia wanaotumia madawa hayo kuachana nayo ni kati ya masuala makuu yanayohitajika katika kupambana na matumzi ya madawa ya kulevya tatizo ambalo limetajwa kuangamzia watu 250,000 kila mwaka.
(SAUTI YA YURI FEDOTOV)