Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia ina matumaini ya kupiga hatua:Ban

Somalia ina matumaini ya kupiga hatua:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Jumatano kwamba Somalia hivi sasa inamatumaini ya kupata fursa ya kuleta mabadiliko. Akizungumza kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Somalia Ban amesema fursa hizo ni za kupiga hatua kubwa kwa upande wa kisheji, kufanya maamuzi muhimu na kufanya mabadiliko, kutofa huduma muhimu kwa jamii na kutekeleza ramani ya amani.

Hata hivyo Ban amesema bado anatiwa hofu kuhusu athari za vikwazo vyovyote vitakavyojitokeza na kuingilia shughuli za misaada kwa watu wa Kusini mwa Somalia. Ametoa wito kwa mara nyingine wa kuruhu mara moja shughuli za utoaji misaada kuendelea na pande zote kujizuia na hatua zozote ambazo zinatishia usalama wa Wasomali na wanaowasaidia.

Amesema mchakato wa amani Somalia unahitaji kuendelezwa  kuratibiwa vyema na ushiriki wa jumuiya ya kimataifa.