Skip to main content

Baraza la Usalama la UM laongeza muda wa ujumbe wa kisiasa nchini Burundi

Baraza la Usalama la UM laongeza muda wa ujumbe wa kisiasa nchini Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu wa ujumbe wa kisiasa nchini Burundi likisisitiza kuwa nchi hiyo ni lazima ipige hatua katika kulinda haki za binadamu, kupigana na ufisadi, kufanyia mabadiliko sekta yake ya ulinzi na kuinua maendeleo ya uchumi.

Kupitia azimio lililopitishwa kwa wingi wa wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliamrisha ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi (BNUB) kuongeza muda huo hadi Februari 15 mwaka 2013. Azimio hilo lilisisitiza kuwa serikali ya Burundi ni lazima iendelee na jitihada zake za kutafuta amani likisema kuwa hatua zimepigwa tangu kumalizika kwa mzozo nchini humo.