Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapata matumaini juu ya kuondoshwa askari watoto kwenye ngome za waasi Jamhuri ya kati

UM wapata matumaini juu ya kuondoshwa askari watoto kwenye ngome za waasi Jamhuri ya kati

Kuna ishara ya matumaini imeanza kuangazia huko Jamhuri ya Kati kufuatia kutiwa saini makubaliano mapya yanayotaka kuondolewa kwa askari watoto kwenze vikisi vya kijeshi.

Mpango huo mpya unaweka zingatio ukitaka watoto zaidi ya 1,500 waliko kwenze vikosi vya waasi waondolewe kwenye maeneo hayo. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na ulinzi wa watoto Radhika Coomaraswamy amesema hatua iliyofikiwa na pande zote zilizokubali kutia saini makubaliano hayo ni ishara njema.

Amesema tayari vikosi vya waasi vimeanza kutekeleza azma hiyo na matumaini yaliyopo mpango huo utatekelezwa kwa wakati.