Skip to main content

Ban ataka kuwe na ufadhili zaidi kwa mfuko wa UM

Ban ataka kuwe na ufadhili zaidi kwa mfuko wa UM

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki – moon ametoa wito wa kuendelea kufadhiliwa kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa unaosaidia nchi zinazojikuamua kutoka kwenye mizozo ili kuijenga amani.

Nguzo ya mfuko huo ni tume ya kuweka amani iliboniwa mwaka 2005 ili kusaidia nchini zilizokumbwa na vita kutorejea tena kwenye mapigano. Akihututubia mkutano wa washikadau kuhusu mfuko huo Ban ameeleza jinsi mfuko huo umesaidia katika kubadili makundi ya waasi nchini Burundi na kuleta uwiano kati ya pande zinazo zozana nchini Sierra Leone.