Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na baraza la usalama vifanyiwe marekebisho:Kabila

UM na baraza la usalama vifanyiwe marekebisho:Kabila

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametoa wito wa kuufanyia marekebisho Umoja wa Mataifa na baraza la usalama la Umoja huo.

Akihutubia katika mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Rais Kabila ameutaka umoja wa Mataifa kuimarisha uongozi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na pia kupanua wigo wa wajumbe wa baraza la usalama ambao kwa sasa ni 15. Jason Nyakuni anaarifu

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Joseph Kabila ametoa wito kwa Umoja wa Matifa kulipa mamlaka zaidi baraza kuu la Umoja wa Matiafa na kuongeza uanachama baraza la usalama ambalo kwa sasa lina wanachama 15.

(CLIP KABILA)

Unachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wa nchi 15 haujabadilika kwa miongo kadha. Baraza hilo linaundwa na wanachama watano wa kudumu wakiwemo Marekani , Urusi , China , Uingereza na Ufaransa walio na kura ya turufu na pia wanachama wengine kumi wasiokuwa na kura ya turufu na pia wasio wa kudumu.